Wednesday, 26 June 2013

NAMNA YA KUANZISHA BIASHARA.....

Ukitaka kufanya biashara yoyote ile unatakiwa kufanya utafiti. Kutokufanya utafiti ni chanzo cha biashara nyingi kuharibika. Lazima ujiulize kwamba unataka kufanya biashara gani? Usiseme unataka kufanya biashara yoyote ile kwani kusema kwamba unataka kufanya biashara yoyote ile ni kupoteza mwelekeo kwa kuwa utakuwa hujui unataka kufanya nini. Kama hujui cha kufanya hakuna kitu utakachokifanya. Hili ni tatizo la watu wengi. Hata baadhi ya watu niliokutana nao wakitaka ushauri wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo hili. Njia ya kukusaidia kuamua ufanye biashara gani ni kwa kujiuliza umewahi kufanya kazi au biashara gani? Umesomea nini? Vipaji vyako ni vipi? Ni biashara ipi au kazi ipi unapenda zaidi kuliko nyingine na kwa sababu gani? Ukisha jiuliza maswali haya chukua kalamu na karatasi uandike maswali yako na kuyajibu. Ukikagua maswali na majibu yako utagundua shughuli unayoipenda, unayoiweza na una kipaji nayo na hiyo ndiyo inayokufaa. Ukishachagua biashara unayoipenda ni rahisi sana kufanikiwa kwani shughuli utazifanya kwa hiyari bila kujilazimisha. Kama unashindwa kuamua ni biashara gani ufanye, soma sura ya sita katika kitabu hiki. Nimeelezea kuhusu mawazo yanayoweza kukusaidia kuanzisha biashara mbalimbali ambazo unaweza kuzifanya. Kama utakuwa bado hujafikia uamuzi baada ya hapo basi tafuta na wasiliana na washauri ili mbadilishane mawazo na ufundishwe jinsi ya kuamua ufanye biashara gani.
Mambo mengine unayotakiwa kuyafanyia utafiti ni:-
 

(i) Kujua siri ya bishara unayotaka kufanya ili upate mbinu za kupata mafanikio. Unaweza kupata siri au kujifunza mbinu kutoka kwa watu wanaofanya biashara kama unayotaka kufanya. Suala hili ni gumu sana kwani wafanyabiashara wengi huwa wanaficha siri za biashara zao ili kulinda wasizidiwe maarifa na washindani wao. Unaweza kuipata siri hiyo kama utakwenda kupata ushauri toka kwa mfanyabiashara ambaye yuko mbali na mahali unapofanyia biashara, au tafuta ushauri kwa wataalamu wa mambo ya biashara.
(ii) Fanya utafiti wa soko la bidhaa unazouza au unazotarajia kuuza. Jiulize, je bidhaa unazotaka kuziuza zina soko? Utawauzia watu gani na utauzaje? Kama wewe ni mzalishaji, una mazao / bidhaa unapaswa kuuza kwa jumla, mchanganyiko ama rejareja? Je utatangaza vipi bidhaa zako? Maelezo ya namna ya kutangaza bidhaa zako utayapata katika Sehemu ya Tatu ya Kitabu hiki. Utafiti wa soko unaweza kuufanya kwa kuwauliza wafanya biashara waliotangulia maswali hayo ya utafiti kwani wao wamekuwapo kwenye soko na wanazijua siri za soko.
(iii) Tengeneza bajeti yako kwa kuorodhesha vitu vinavyohitajika na gharama zake ili kuweza kuanzisha biashara yako. Vitu hivyo ni:-
(a) Gharama za Kujenga au kupanga ofisi
(b) Gharama za Leseni ya biashara
(c) Makadirio ya kodi toka TRA
(d) Garama ya vifaa vya ofisi yaani, Samani, makaratasi, mitambo, mashine, nk
(e) Manunuzi ya malighafi au bidhaa za kuanzia biashara
(f) Idadi ya wafanyakazi na gharama za mishahara yao.
(g) Gharama nyinginezo kama vile, umeme, maji, nk.
(iv) Unatakiwa kujua ni mtaji kiasi gani unahitajika kuanzisha biashara yako. Mtaji huo utaujua baada ya kujumlisha gharama zilizoorodheshwa katika kupengele namba (iii)Gharama hizi ni za mwaka ule wa kwanza wa kuanzia
(v) Tafuta Mtaji.
Mtaji unaweza kupatikana kutoka kwenye vyanzo vifuatavyo:-
(a) Akiba au mshahara
(b) Msaada au mkopo kutoka kwa ndugu na jamaa.
(c) Kuingia ubia na mtu mwenye mtaji
(d) Mkopo toka baadhi ya asasi kama vyama vya akiba na mikopo (SACCOS), NGO za kifedha sipokuwa Benki kwani hizi huwa hazitoi mikopo kwa mtu anayeanzisha biashara.

TARATIBU ZA KISHERIA ZA KUFUATA ILI KUANZISHA BIASHARA
Baada ya kufanya utafiti na kupanga mipango ya kuanzisha biashara unatakiwa kwanza kuangalia taratibu za kisheria ambazo unatakiwa kuzifuata na kuzitekeleza. Kama biashara yako ni ndogo anza kama mtu binafsi. Faida ya kuanza biashara kama mtu binafsi ni urahisi wa kuanzisha biashara; urahisi na wepesi wa kutoa maamuzi kwani huhitaji ridhaa ya mtu mwingine kabla ya kutoa uamuzi; mtaji unaohitajika utakuwa mdogo kutokana na gharama za uendeshaji kuwa ndogo, biashara hii inaweza kuendeshwa kwa msaada wa familia kwa kumtumia mke au mume, watoto au ndugu na jamaa na raslimali za familia kama nyumba na samani. Unapoanzisha biashara na kuiendesha mwenyewe unakuwa huru tofauti na mifumo mingine. Matatizo ya kufanya biashara kama mtu binafsi ni:- Kushindwa kupanua biashara yako kwa ufinyu wa mtaji; kufilisiwa mali zako za binafsi iwapo biashara yako itafilisika kwani katika mfumo huu mali ya biashara na mali binafsi si rahisi kuzitenganisha; Kuongeza mtaji inakuwa ni vigumu, hivyo unaweza kushindwa kupanua biashara yako. Ili kuepukana na matatizo niliyoyataja hapo juu unaweza kuungana na watu wengine kufanya biashara kwa ubia. Faida za kufanya biashara kwa ubia ni: Kupata fursa ya kuongeza mtaji kwa kushirikiana na wafanyabiashara wengine ambao wataleta mitaji yao; Kuongeza ujuzi katika shughuli kwa kuleta wataalamu pale taaluma Fulani inapohitajika. Matatizo ya kuendesha biashara kwa njia ya ubia ni: Kufilisiwa mali zako binafsi endapo biashara yako itafilisika; kudhulumiana mali endapo moja wa wabia atakuwa si mwaminifu ambapo anaweza kuingia mikataba mibovu na kusababisha hasara ambayo itabebwa na wabia wote. Ni muhimu kuwachunguza watu tunaotaka kujiunga nao ili tujue kama ni waaminifu. Pia ni vyema kuwapo na mkataba wa maandishi mnapoanzisha biashara ya ubia mkimshirikisha mwanasheria kama shahidi ili kujikinga na kudhulumiana; Kufariki kwa mbia mmoja kunaweza kusababisha kuvunjika kwa ubia; kotokuelewana kwa wabia kunaweza kusababisha kuvunjika kwa ubia. Kama biashara ikikua unaweza kuanzisha kampuni. Mfumo wa uendeshaji wa kampuni unazo faida zifuatazo: unatenganisha majukumu ya wamiliki mali na kampuni yaani kampuni inaposajiliwa inakuwa inakuwa na hadhi na kutambulika kisheria kama ni mfumo tofauti na wamiliki. Mfumo huu unatenganisha majukumu kati ya menejimenti na wamiliki wa kampuni; madeni ya kampuni yatalipwa hadi kufikia kikomo cha mtaji uliowekezwa na wamiliki. Hivyo, mali binafsi za wamiliki wa kampuni haziwezi kukamatwa kufidia madeni ya kampuni endapo kampuni itafilisika. Mfumo wa kampuni unatoa nafasi ya kupanua mtaji kwa kukusanya mitaji kwa kuongeza wanahisa au kupitia soko la mitaji ya hisa. Mfumo huu ndiyo unafaa kwa biashara kubwa kwani unatoa nafasi ya kupanuka kwa biashara na kuendelea kuwapo kwa biashara hata kama baadhi ya wamiliki wake wakifa au kujitoa katika kampuni.
Mambo ya muhimu ya kutekeleza kisheria kabla ya kuanzisha biashara ni:-
(a) Kuwa na ofisi
(b) Kukata leseni
(c) Kusajiliwa na TRA kama mlipokodi na kupewa namba ya mlipakodi
(d) Kufanyiwa makadirio ya kodi ya mapato ya awali
(e) Kutimiza masharti mengine ya keshiria kuwa mfano kama wewe unataka kufanya biashara ya ukandarasi wa ujenzi wa majengo lazima usajiliwe kwenye Bodi ya Wakandarasi.
Kama unafanya biashara ya kati au kubwa unapaswa kufuata sheria. Ni makosa kufanya biashara bila kufuata sheria za nchi. Hata hivyo, kuna biashara zingine ndogo ndogo sana kiasi kwamba uanzishaji wake si rahisi kufuata sheria hizo hapo juu, mfano uuzaji wa maandazi, karanga na vitu vingine vidogovidogo. Hizi zinaitwa biashara zisizo rasmi au biashara ndogondogo. Ni vyema ukachunguza kama biashara unayoifanya ni ndogo au kubwa ili ujue kama unapaswa kufuata taratibu za kisheria au la, kwani kutokujua utaratibu na sheria siyo kinga ya kukufanya usishitakiwe.

Know The Benefits of Using Body Spa Salt....


A salt body scrub is a beauty product made by combining a course salt with oil. Some of the most commonly used salts found in salt body scrubs are sea salt and Epsom salts. These varieties of salt are purified enough to be gentle on the skin; regular table salt should never be used, as it is too harsh. If the skin is too sensitive for any salts, sugar can be substituted to achieve a similar effect. Light-textured oils such as jojoba, almond, and grapeseed work best to mix with the salts.

There are several benefits to using a salt body scrub. When the scrub is rubbed over the skin, it removes the surface layer of dead skin cells. After it is rinsed off, the newer, younger skin cells are left on the surface, giving the skin a smooth feel and youthful appearance. In addition to the external physical benefits, the salt helps open pores and draw out toxins. The act of massaging the body salt scrub into the skin increases circulation, relaxes muscles, and helps alleviate tension.

Salt body scrubs can be used at home or can be administered by a therapist at a spa. When listed on spa menus, the treatment can also be called a salt glow or body polish. The salt body scrub treatment at a spa will sometimes be followed with a Vichy shower. A Vichy shower contains five to seven shower heads in a row that are turned on above the treatment table to rinse the scrub off without the client having to move or get up from the table. The treatment is then usually finished off with a lotion massage to seal the moisture into the skin.

If applying a salt body scrub as a home treatment, the skin should be moistened before the scrub is applied. The body scrub should then be rubbed in for at least 1 minute to get a complete exfoliation. Gentle pressure should be used so as not to irritate the skin. Salt body scrubs work exceptionally well on tougher body parts, like elbows, knees, and feet, but should not be used on more delicate areas, like the face. The scrub can be used once a week to keep skin smooth and soft.

They are available at Ng'ariNg'ari, Sinza Mapambano. Call 0654450200

Umuhimu wa Mafuta ya Karafuu,Sabuni ya Karafuu na Unga wa Karafuu

Mafuta ya Karafuu
 
 Mafuta karafuu ni mazuri sana kwa kuchulia mwili pale unapouma.

Sabuni ya karafuu
 
 Tumia sabuni ya karafuuu kujikinga na kuondoa matatizo mbalimbali ya ngozi,kama chunusi na vipele.

Unga Wa Karafuu

Unga wa karafuu unatumika kusugulia mwili,utauchanganya na maji ya rose au mafuta ya mzaituni.

Unga wa karafuu Tunauza 2000,Sabuni ya karafuu 3000 na Mafuta ya karafuu 3000
Karibu sana Ng'ariNg'ari ujipatie Vipodozi Asilia (0654450200)

Friday, 21 June 2013

Mambo Yanayosabisha Biashara Ishindwe Kustawi



Kuna sababu nyingi zinazosababisha biashara kushindwa kuendelea na hatimaye kufa. Sababu tatu kuu zinazokwamisha biashara kuendelea, kwanza ni sababu binafsi za mjasiriamali, sababu za kibiashara, na sababu za mazingira.

1.Sababu binafsi za mjasiriamali. Tafiti nyingi zimebainisha kwamba mjasiriamali anachangia kufanikiwa kwa biashara au kushindwa. Umri, uzoefu, aina ya biashara  unayoifanya, historia ya familia, na kiwango cha elimu pia inachangia biashara kufanya vizuri au kushindwa kushamiri. Pia ukosefu wa ari ya mafanikio na kutojituma kufanya kazi kwa bidii ni sababu nyingine. Tafiti pia zinaonyesha kuwa mjasiriamali yeyote ambaye hajawahi kuwa kiongozi popote pale ana uwezekano mkubwa wa kushindwa kusimamia biashara ukilinganisha na mtu ambaye amewahi kuwa kiongozi shuleni au katika vikundi mbalimbali kwa mfano, jumuiya za kidini.

Kwa upande mwingine, tafiti zinaonyesha kwamba biashara zinazoanzishwa na kuendeshwa na mtu mmoja zina nafasi kubwa ya kutofanikiwa ukilinganisha na biashara zinazoendeshwa na mtu zaidi ya mmoja.

Ushauri, ili uweze kufanikiwa katika biashara kubali kushika nafasi za uongozi sehemu yoyote iwe kwa mwanafunzi shuleni au chuoni, iwe katika jamii na jumuiya za dini, kwani inaaminika kwamba ukiweza kuongoza watu ni rahisi kuendesha na kuitawala biashara yako.

Pia ubunifu na kujenga ari ya kujituma husaidia biashara kukua, kama umeweka msimamizi wa biashara hakikisha kila siku unapata taarifa muhimu juu ya mwenendo wa biashara hata kwa njia ya ujumbe mfupi wa meseji.

2.Sababu za kibiashara. Sababu za kibiashara zinajumuisha ubora wa bidhaa au huduma, wateja na soko kwa ujumla. Tafiti pia zinabainisha kuwa anayefanya biashara bila kufuata kanuni za kimasoko mfano huduma kwa wateja, bei, sehemu ya biashara, ana nafasi kubwa ya kushindwa katika biashara.

Pia biashara zinazoanzishwa kwa mtaji mdogo kulinganisha na mahitaji halisi hua zinakosa takwimu sahihi za biashara na hazina kumbukumbu za mahesabu na mwisho wa siku zinakosa mtaji kidogo uliokuwapo. Biashara zinazoendeshwa bila kupata ushauri wa kitalaam zina uwezekano mkubwa wa kufa mapema.

3.Sababu za mazingira. Sababu za mazingira zinahusisha biashara za kuiga, ushindani mkali katika soko na kupanda haraka kwa gharama za uzalishaji.

Mjasiriamali kushindwa kuendesha biashara ni fursa ya kufanikiwa kwa biashara nyingine kutokana na ukweli kwamba mjasiriamali hujifunza kutokana na makosa mbalimbali.

Kama  atarekebisha makosa na kuanza upya biashara ya awali au kubadilisha biashara kuna uwezekano mkubwa wa kufanikiwa.

Endapo mjasiriamali anashindwa kuendesha  biashara, inatoa ishara kuwa kuna kitu hakiko sawa hivyo marekebisho anapaswa kufanya marekebisho na  kuangalia upya vihatarishi vya biashara na kuamua namna ya kufanya ili kuvipunguza. Jenga urafiki na watalaamu mbalimbali ufaidi ushauri wao kuboresha biashara yako.



Wednesday, 5 June 2013

Mafuta ya mimea Asilia kwa Ubora wa Nywele yako....


Shantalle Herbs Oil ni mafuta ya maji yenye mchanganyiko wa mbegu za mmea wa asili wenye virutubishovya hali ya juu, huzuia kukatika nywele na kuifanya ngozi yako isiwe kavu ,huotesha kwa muda mfupi na kujaza nywele,na kurudi katika khali ya kawaida wale wenye matatizo ya kichwa pia husaidia unaweza ukafanyia stiming na masaji ya kichwa ambayo inaweza kufungua mishipa ya fahamu . Tunapatikana Tabata Relini nyuma ya chuo cha walimu St. Marry's, kinondoni Bantu Saloon, Ng'ariNg'ari sinza Mapambabo,Congo cosmetic Kinondoni,studio. Magomeni kondoa JJ saloon. kwa maelezo zaidi Tupigie 0766 291 947, 0652 048 512




Kongamano na Maonyesho ya WAJASIRIAMALI KUMEKUCHA 02 June












Napenda kutoa shukurani zangu za Dhati kwa wote walioweza kufika kwenye Kongamano na Maonyesho haya ya WAJASIRIAMALI KUMEKUCHA ambayo yanafanyika mara mbili kwa mwaka. Hizi ndio fursa za kujitangaza,kuuza na kujifunza, so usiwe unakubali kukosa. For more info plz call me 0753643934

Thursday, 16 May 2013

Mtaji wa Biashara

Mtaji ni nini? Je, mtaji ndio kianzo pekee cha biashara? Je ni mitaji ya aina ngapi mtu anahitaji kuweza kufanikisha biashara? Jee ni pesa peke yake? Majibu ni kwamba; Watu wengi wana mitaji lakini pengine hawajui kama wanayo. Mtaji sio pesa pekee. Mtaji unaweza kuwa akili yako au kiwango fulani cha pesa cha kukuza au kujenga biashara yako. Pia mali zinaweza kuwa mtaji wako na kuifanya biashara yako ikue. Hata hivyo huhitaji pesa taslimu pekeyake kuifanya biashara yako ikue. Unaweza kutumia mali zako kama nyumba yenye hati kuweka dhamana ya mkopo benki kupata pesa za kuendesha na kukuza biashara yako.

Ili Kuanzisha biashara yeyote lazima mtaji unahitajika unaweza kuwa, fedha au akili yako na mbinu zako. Wakati mwingine akili yako au ubunifu wako unaweza kuwa ndiyo mtaji pekee hasa katika kazi zinazohitaji utaalamu fulani. Kama nilivyo eleza hapo juu mtaji sio lazima uwe pesa taslimu, ila mali ulionayo au akiliyako pia nayo ni mtaji wako. Mambo haya yanategemeana na unataka kufanya biashara ya aina gani. Kuna aina za mitaji zifuatazo katika biashara;-

a) Mtaji unaotokana na rasilimali watu: Huu ni ujuzi au kipaji cha mtu mwenyewe. Mtaji huu huwa unaandaliwa na mhusika mwenyewe kwa kusoma kufanya mazoezi na kupata ujuzi ambao utamuwezesha kukubalika katika jamii na kumuingizia kipato na kumpatia utajiri yeye mwenyewe au Kampuni yake. Aina hii ya mtaji inatofautishwa na nguvu kazi inayotumika kwenye ajira ambayo ni uwezo wa kufanya kazi. Mtaji huu hujulikana pia kama kipaji.

 
b) Mtaji wa pesa: Hizi ni pesa zinazotumika kuijenga au kupanua biashara ili iijiendeshe.

c) Mtaji unaotokana na ubunifu: Mtaji kama huu unatumiwa sana na wasanii pamoja na wajasiriamali wengine. Wimbo ukitoka na ukapata soko kubwa. nani mwenye wimbo hapa. Je ni mtunzi? mwimbaji? au mzalishaji? Hapa mwenye wimbo ni mtunzi, mwisho wa siku anaepata pesa zaidi ni mtunzi au sio jamani? Hivyo mtaji unaotokana na ubunifu unaweza kuwa ni unatokana na hakimiliki ya kitu,wimbo, bidhaa au kitu kinachofanana na hicho. Mfano AZAM alipo anza kutengeneza unga wa ngano unga wake ulipata soko sana. Baadae akaibuka AZANIA, ambaye jina lake hilo kwa haraka unaweza ukadhania nikampuni moja. Hata wewe ukianzisha biashara yako ya unga unaweza kuupatia jina la AZAN utauza sana tu!

d) Mtaji wa bidhaa au mashine za kuzalishia bidhaa: Mtaji huu unatokana na kifaa kama mashine ya kutengeneza bidhaa fulani za kuuza. Mfano; kama wewe ni mwandishi, mashine unayotumia ni kompyuta, mashine ya kuchapishia, kalamu na karatasi. Mtaji huu ni tofauti na mtaji wa pesa. Thamani ya mtaji huu ni jinsi unavyowweza kukuzalishia mali au bidhaa
Jee mtaji unaweza kupatikana vipi?

Mtaji unaweza kupatikana kutoka kwenye vyanzo vifuatavyo:-

(a) Akiba au mshahara
(b) Msaada au mkopo kutoka kwa ndugu na jamaa.
(c) Kuingia ubia na mtu mwenye mtaji
(d) Mkopo toka baadhi ya asasi kama vyama vya akiba na mikopo (SACCOS), NGO za kifedha, isipokuwa Benki kwani hizi huwa hazitoi mikopo kwa mtu anayeanzisha biashara.

Kitu cha muhimu kabisa ni kuwa na wazo zuri la biashara na mpango wa biashara ulio mzuri pamoja na utayari wako wewe mhusika kuifanya hiyo biashara, masuala ya mtaji wa pesa hufuata badae. Jambo la kwanza kabisa unalolihitaji ni utashi wa kufanya mradi au bishara yako, pili ni imani kwa hilo unalotaka kulifanya, ukiweza kuunganisha utashi na na imani kua utaweza basi ujue unaelekea kwenye mafanikio. Kitu kingine muhimu ubunifu ambao unaugawa katika njia mbili kwa kuangalia wengine wanafanya nini na wewe ufanye kama wao. Pia unaweza kufanya utundu wa kubuni kitu kipya ambacho hakijawahi kufanywa na mtu mwingine yeyote. Ni muhimu kuwa na ujuzi maalumu, hapo ni kwamba nilazima uijue vizuri biashara unayotaka kuifanya uliza walioweza kufanya buiashara hiyo vizuri pia pata maelezo ya kutosha jinsi ya upatikanaji wa bidhaa,wateja,masoko pamoja na mambo ya kodi. Jambo jingine ni kuwa na mipango ambayo ni madhubuti, hapo sasa ndio unaandaa makadirio ya mapato na matumizi kama kianzio. Tengeneza bajeti yako kwa kuorodhesha vitu vinavyohitajika na gharama zake ili kuweza kuanzisha biashara yako. Vitu hivyo ni:-


(a) Gharama za Kujenga au kupanga ofisi
(b) Gharama za Leseni ya biashara
(c) Makadirio ya kodi toka TRA
(d)Garama ya vifaa vya ofisi yaani, makaratasi, mitambo, mashine, nk
(e) Manunuzi ya malighafi au bidhaa za kuanzia biashara
(f) Idadi ya wafanyakazi na gharama za mishahara yao.
(g) Gharama nyinginezo kama vile, umeme, maji, nk.

Unatakiwa kujua ni mtaji kiasi gani unahitajika kuanzisha biashara yako. Mtaji huo utaujua baada ya kujumlisha gharama zilizoorodheshwa katika kupengele (a) mpaka (g) hapo juu.Gharama hizi ni za mwaka ule wa kwanza wa kuanzia pamoja na jinsi gani utapata pesa za kuwekeza ambazo unaweza kutoa kwenye akiba zako kutokana na mapato yako huko nyuma ,au ukaomba mkopo kutoka benki au kwa mtu yoyote atakae kuamini japo hapa kwetu ni vigumu kuomba mkopo uende kuanzisha biashara labda uende kukopa saccos. Baada ya hapo ndipo unafikia uamuzi wa lini utaanza mradi wako tena bila kupoteza muda.